Nyumba ya Wageni Mbutusyo
Nyumba ya Wageni Mbutusyo
Nyumba ya Wageni ya Mbutusyo ilianzishwa na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini. Ni jengo zuri la muda mrefu, lililokarabatiwa mwaka 2017 tangu wakati huo ni mojawapo ya mahali bora zaidi pa kukaa wilayani Rungwe. Eneo tulivu lililoizunguka nyumba ya wageni na umuhimu wa historia ya mkoa vitakupatia maarifa ya kipekee.
Kanisa la
kwanza kabisa lililojengwa na Wamisionari wa Kanisa la Moravian nchini Tanzania
lipo mita chache tu kutoka nyumba ya wageni. Kwa watu
wanaovutiwa na historia ya wamisionari na wilaya ya Rungwe, kuna jengo la Nyaraka na Makumbusho Rungwe, karibu kabisa na nyumba ya wageni Mbutusyo.
- Chumba
cha kitanda kimoja (single bedroom) - Tsh.
50,000 kwa usiku
- Chumba
cha vitanda viwili (double bedroom) - Tsh. 60,000
kwa usiku
- Chumba
cha vitanda viwili (twin bedroom) - Tsh. 60,000
kwa usiku
Pia, tunatoza
shilingi 20,000 kwa siku kwa ajili ya malipo ya Mhudumu anayefanya usafi. Hata
hivyo, kiasi hicho kinagawanywa kati ya wageni wote wanaoishi katika nyumba ya
wageni ya Mbutusyo.
Bei ya chakula
- Chakula cha asubuhi Tsh. 5,000
- Chakula cha mchana Tsh. 15,000
- Chakula cha jioni Tsh. 15,000
Milo yetu inatayarishwa
kwa kutumia bidhaa za ndani, tunaweza kuandaa chakula chochote kulingana na
upendeleo wa mteja.
Chumba chetu cha chakula
Eneo la nje la kupumzika
Mawasiliano
Nyumba ya Wageni Mbutusyo
S.L.P. 32
Tukuyu
Mbeya Region
Tanzania
Barua Pepe: butusyoguest@gmail.com
liliemanuel@gmail.com
butusyoguest@gmail.com
Simu: +255 764 934339
+255 748 104700