Hospitali ya Isoko
Hospitali ya Isoko, ni Hospitali teule ya wilaya ya Ileje tangu 1976, inamilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini. Ilijengwa na Kanisa la Moravian jimbo la Kusini mwa Tanganyika kwa msaada kutoka Kanisa la Moravian Ulaya. Hospitali ilianza kama zahati miaka ya 1950 na ikawa Hospitali mwaka 1961. Ilianza na vitanda 50 na baadaye ilipanuliwa mwaka 1976 ikawa na vitanda 110. Siku hizi, Hospitali ina vitanda 122 na huajiri jumla ya watu wapatao 90. Hospitali ilisaini mkataba wa huduma na wilaya ya Ileje mwaka 2012.
Hospitali inapatikana kijiji cha Isoko, kata ya Kafule, tarafa ya Bundali, wilaya ya Ileje katika mkoa wa Mbeya. Hospitali iko pembezoni mwa mlima Kashima, ambao ni mlima mrefu zaidi katika wilaya. Mlima umezungukwa na uoto wa asili, ambao una mazingira mazuri na tulivu katika kijiji cha Isoko kwa mwaka mzima.
Hospitali ya
Isoko iko umbali wa kilomita 200 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na
Hospitali ya kanda, kilomita 65 kutoka Hospitali ya Itumba na makao makuu ya
wilaya na kilomita 65 kutoka makao makuu ya wilaya ya Rungwe.
Daktari mkuu | Dr. Mashaka
Shibanda |
Katibu
wa afya | Mr.
Zacharia Kangele |
Muuguzi mkuu | Ms.
Asha Konki |
Katibu
msaidizi wa afya | Mr.
S. Mlwafu |
Mfamasia | Mr.
Joseph Kajange |
Mhasibu | Mr.
Norbert Dickson |
Muundo wa shirika
Muundo wa shirika
Surgical Department | Operating Theatre, male- and female Surgical Ward |
Internal Medicine | Male- and female medical ward |
Paediatric | Paediatric ward |
Obstetrics and Gynaecology | Labour room |
Antenatal ward | |
Postnatal ward | |
Neonatal ward | |
Pharmacy | Dispensing |
Pharmacy store | |
Radiology | Ultra sound |
X-Ray | |
Laboratory | Clinical laboratory |
Mortuary | |
Administration | Medical record |
Registry | |
Accounting | |
General Store (procurement) | |
Workshop (Medical engineering) | |
Workshop (others) | |
Orthopaedic | Orthopaedic |
Physiotherapy | |
Psychiatric | Psychiatric |
Pharmacy | Dispensing |
Pharmacy store | |
Radiology | Ultra sound |
X-Ray |
Idadi ya wagonjwa
Jedwali
lifuatalo linaonyesha kazi ya Hospitali ya Isoko kati ya mwaka 2010 na mwaka 2014.
DESCRIPTION |
2010 |
2011 |
2012 |
2013 |
2014 |
Mahudhurio ya wagonjwa wa nje (OPD) |
19,743 |
20,431 |
22,942 |
14,882 |
10,417 |
Mahudhurio ya afya ya uzazi wa mtoto |
434 |
516 |
643 |
|
5,881 |
Mahudhurio ya watoto chini ya miaka mitanomitano |
9,598 |
2,024 |
939 |
7,231 |
988 |
Kliniki ya wajawazito |
878 |
1,339 |
989 |
586 |
740 |
Family planning |
2,015 |
1,758 |
2,032 |
2,383 |
1,078 |
Wastani wa wagonjwa wa nje kila siku |
50-60 |
60 |
60 |
51 |
29 |
Idadi ya wagonjwa waliolazwa |
5,355 |
3,297 |
4,303 |
3,874 |
3,914 |
Waliojifungua |
725 |
52 |
632 |
579 |
801 |
Upasuaji mkubwa |
180 |
202 |
211 |
383 |
183 |
Upasuaji mdogo |
360 |
422 |
344 |
394 |
240 |
Uchunguzi wa kimaabara |
14,113 |
11,189 |
13,028 |
13,244 |
17,299 |
X –ray zilizochukuliwa |
831 |
706 |
764 |
640 |
357 |
Kitengo cha meno |
37 |
316 |
541 |
754 |
796 |
Mtazamo
Kuwa watoa huduma bora wa afya zenye ubora na gharama nafuu, kwa kuzingatia maadili ya kibinadamu.
Mission
Provide quality, affordable and accessible health care services to all the people in the area with high professional care for social economic sustainability.
Lengo
Kutoa huduma bora za afya, bei nafuu na zinazopatikana kwa watu wote katika eneo hilo na huduma ya juu ya kitaaluma kwa ustawi wa kiuchumi wa jamii.
Maadili
Upendo - Tunasisitiza upendo wa kindugu kati ya watu.
Uadilifu - Nidhamu ya juu katika kukamilisha kazi.
Uaminifu - Kama kituo cha kanisa tuna uaminifu mkubwa kwa jamii yetu.
Utawala Bora - Tunatoa huduma zetu kwa kuzingatia kanuni za utawala bora.
Mradi wa
Watoto yatima - Mpango wa kituo cha watoto yatima Isoko ulianza mwaka 1996,
baada ya kusaini makubaliano kati ya Dinari ya Berg Strass - Mitte nchini
Ujerumani na Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini.
Malengo makuu
ya mradi ni kuwasaidia watoto yatima kwa mahitaji kama nguo, matandiko, ada ya
shule na huduma za matibabu. Kati ya mwaka 2012 na mwaka 2014, wastani kwa
mwaka watoto yatima wapatao 171 walisaidiwa.
Mradi wa Artemisia - Mradi wa dawa za asili wa mmea artemisia ulianzishwa na Mission 21 tangu mwaka 2008. Inahudumia watu vijijini, maeneo ya mbali ya MCT-SP. Mradi unalenga kupunguza magonjwa yaliyopo katika jamii. Mmea mkuu ni Artemisia, ambao unaimarisha kinga za mwili dhidi ya malaria kwa njia ya asili.
Shughuli za kuongeza kipato
Msitu - Hospitali inamiliki hekta 40 za msitu zenye misonobari 46,502 katika kijiji cha Nachibughubughu-Mbangala. Ni moja ya misitu bora zaidi na iliyopandwa sana katika wilaya.
Nyumba ya mapumziko - Hospitali hutumia jengo moja kama nyumba ya mapumziko. Ina vyumba sita na ukumbi mdogo. Ni nyumba ya thamani, ambayo viongozi wengi wa serikali huitumia kwa kulala na kufanya mikutano, semina na warsha.
Mgahawa - Hospitali inamiliki mgahawa mdogo. Wateja wake ni wafanyakazi wa hospitali, ndugu wa wagonjwa na wageni wa hospitali. Kwa sasa, hospitali huhudumia chakula cha asubuhi na cha mchana.
Karakana ya useremala – Karakana ya useremala iko katika eneo la hospitali. Karakana hiyo ina vifaa na mashine za kukatia. Karakana inawezesha utekelezaji wa shughuli za hospitali kama vile ukarabati na urekebishaji wa majengo ya hospitali.
Mashine za kuchongea na kukatia - Mashine hufanya kazi na umeme. Wakati wa kiangazi mashine hazifanyi kazi kutokana na uzalishaji mdogo wa nishati wa maji.
Nyumba ya
wauguzi wa wagonjwa - Nyumba ya wauguzi ina hosteli mbili, moja kwa wanawake na
nyingine kwa wanaume. Pia kuna jiko, ambalo wauguzi hutumia kuandaa chakula cha
wagonjwa.
Hospitali ya Isoko
S.L.P. 1
Isoko-Ileje
Tanzania
Barua Pepe: isokohospital6@gmail.com
Simu:
Daktari
mkuu +255 754 915622
Katibu
wa afya +255 755 052726