Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian
Chuo cha
Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian kilianzishwa mwezi Februari 2002 na mkuu wake
wa kwanza Michael Kajuni na Kanisa la Moravian Tanzania –jimbo la Kusini.
Nambari yake ya hati ya usajili ni VET / MBY / PR / 2012 / C / 043. Chuo
kilianza na wanafunzi wachache na kozi mbili tu, ushonaji, ufundi seremala na
uundaji. Wanafunzi wapatao 110 wanasoma Kyela VTC na tunatoa kozi mbali
mbali za muda mdefu na muda mfupi:
Kozi za muda mrefu (miaka 2):
- Useremala na uundaji
- Ushonaji
- Ufungaji wa umeme wa majumbani
- Ufundi wa magari
- Mafunzo ya kompyuta (takriban miezi 2)
- Udereva (wiki 5)
Vifaa
Tunatoa
vifaa mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi
wetu. Miongoni mwa vifaa hivyo ni maabara ya kompyuta yenye kompyuta zipatazo
22, madarasa mawili yenye vifaa vya ushonaji, karakana mbili kwa ajili ya wanafunzi
wa useremala, na karakana ya ufundi wa
magari. Pia tuna bweni kwa wasichana, ambalo linawawezesha kukaa chuoni. Bweni
lina nafasi kwa wanafunzi 36.
Wafanyakazi
Mkuu | Mhasibu | Mtaaluma mkuu |
Michael Kajuni- +255 764 103046 | Happy Kalinga - +255764 476666 | Christopher Selemani - +255764 476666 |
Mawasiliano
Chuo cha
Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian
Kyela-Mbeya
Tanzania
Simu: +255 764 103046
Barua Pepe: kyelamoravianvtc@gmail.com