Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Rungwe Moravian
Chuo cha Rungwe VTC kilianzishwa na
wamisionari mwaka 1903, ambacho ni chuo cha zamani zaidi cha mafunzo ya ufundi
nchini Tanzania. Hapo mwanzo, hesabu rahisi na ujuzi wa vitendo wa namna ya kujenga
nyumba ulifundishwa. Hata hivyo, kwa miaka mingi, masomo ya msingi zaidi na
masomo ya ziada yaliongezwa. Chuo kilisajiliwa rasmi na serikali ya Tanzania mwaka
1976, na kupata namba ya usajili 00057. Chuo cha Rungwe VTC kinafanya Mitihani
ya Taifa ya Msingi (National Based Exams) na Tathmini ya Msingi ya Uwezo
(Competence Based Assessments). Kwa kuzingatia ukweli, kwamba chuo cha Rungwe VTC kimekuwa kwa zaidi ya
miaka 100, hatuna budi kusema kwamba chuo kimekuwa na mchango mkubwa katika
maendeleo ya mkoa na Tanzania kwa ujumla, na tutaendelea kufanya hivyo. Chuo
hasa kinahamasisha na kuwasaidia watoto yatima kupata elimu ya mafunzo ya ufundi,
na wahitimu wote hupewa vifaa muhimu, vinavyowawezesha kuanza biashara zao
wenyewe.
Chuo cha Rungwe VTC kinatoa kozi zifuatazo:
- Ufundi wa magari
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ushonaji na ubunifu wa mavazi
- Useremala na uundaji
- Ufundi Umeme wa Jua (Solar Electrical Installation)
-
Sayansi ya Uhandisi
Hisabati
Mafunzo ya Kompyuta
Ubunifu wa michoro
Kiingereza
Ujuzi wa Mawasiliano
Ujuzi wa maisha
Ujasiriamali
Mpaka sasa Chuo hiki kinapokea Wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali wanaojiunga na chuo hiki.
Vifaa
Mara kwa
mara tunaboresha miundombinu yetu kwa ajili ya mazingira bora ya kujifunzia.
Hata hivyo, kuna vifaa ambavyo tunatoa. Kuna karakana kwa ajili ya wanafunzi
wetu wa useremala, darasa lenye mashine za kushonea, chumba cha kompyuta,
karakana ya ufundi wa magari na mabweni mawili. Chuo kinatoa malazi, bweni la
wasichana wanafunzi 60 na la wavulana wanafunzi 40.
Wafanyakazi
Chuo cha
Rungwe VTC kimeajiri walimu 14 ambao hutoa mafunzo ya masomo mbali mbali, na
baadhi ya wafanyakazi wengine wasio walimu. Utawala una watu wafuatayo:
Mkuu wa Chuo
| Gwantwa J. Mwandoloma | jgwantwa@gmail.com +255621448990 / +255766609807 |
Mratibu wa Mafunzo
| ||
Karani/ Keshia | Upendo J. Kayuni | kayunipendo47@gmail.com +255682409114/+255626505394 |
Mawasiliano
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Rungwe Moravian
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania
Simu: +255 621-448 990
mail : jgwantwa@gmail.com