Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Ileje Moravian
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Ileje kipo katika kijiji cha Isongole, karibu na mpaka wa Malawi, wilayani Ileje. Chuo hicho kilianzishwa mwaka 2006 na Kanisa la Moravian – jimbo la Kusini mwa Tanzania, kwa msaada wa ZZg (Zeister Zending Genootschap) kutoka Holland.Tunatoa kozi zifuatazo:
Kozi za muda mrefu (miaka 2):
- Ufundi seremala na uundaji
- Ushonaji
- Ufungaji wa Umeme wa majumbani
Kozi za muda mfupi:
- Kozi ya Kompyuta
- Ufungaji wa Umeme wa majumbani
Vifaa
Tunatoa vifaa mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi wetu. Miongoni mwa vifaa hivyo ni maabara ya kompyuta yenye kompyuta zipatazo 15, karakana kubwa kwa ajili ya wanafunzi wa ufundi seremala na uundaji, karakana ya ushonaji yenye vifaa na mashine za kushonea, na darasa maalumu kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa ufundi umeme wa majumbani.Wafanyakazi
Sasa, walimu wanne wa muda mrefu na wafanyakazi wengine wa ziada wanafanya kazi katika chuo cha Ileje VTC.Mkuu | Mratibu
wa Mafunzo |
Jimistone
Mlalila |
Ambokile Kandonga |
Kauli mbiu ya Shule
"Mpe urithi mwanao elimu ya ufundi."
"Fordward the heritage of vocational education to your children"
Mawasiliano
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Ileje Moravian
S.L.P. 150
Isongole-Ileje
Songwe Region
Tanzania
Simu: +255 762 552603