Idara ya Habari
Idara ya habari ya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini ilianzishwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2022 baada ya Mkutano Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini uliofanyika December 2021 kuridhia uanzishwaji wake katika Sinodi ya mwaka huo.
MALENGO YA KUANZISHWA KWAKE.
Idara hii ya habari ilianzishwa kwa malengo yafuatayo.
1. Kukusanya, kuandika na kusambaza habari mbalimbali picha na Video zinazohusu Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini.
2. Kusimamia utoji wa machapisho mbalimbali ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini.
3. Kusimamia na kudhibiti habari zote za Kanisa kutoka kwa utaratibu maalumu
· Kutokana na kukua kwa teknolojia, habari nyingi za Kanisa zimekuwa zikivuja kiholela na kusababisha watu kukosa ukweli kutoka katika kanisa lao na kusababisha kuhangaika kupata taarifa kutoka katika vyanzo visivyo na uhakika. Idara hii ilianzishwa ili kuhakikisha watu wanapata habari za uhakika kutoka vyanzo vyenye uhakika na kudhibiti kuvuja kwa taarifa.
4. Kusimamia na kuratibu uanzishwaji wa Vyombo vya habari vya Kanisa.
· Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini limebeba maono ya kuanzisha vyombo vyake vya habari ikiwemo Radio na Television. Hivyo basi Idara hii ilianzishwa ili kusimamia mchakato mzima wa uanzishwaji na uratibu wa vyombo hivi.
5. Kuanzisha na Kuendesha Kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Kanisa.
· Ukuaji wa teknolojia umesababisha jamii kubwa kupata taarifa zake kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, kwa mantiki hiyo Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini liliona ni vema pia kuifikia jamii kubwa iliyoko mitandaoni kwa kuanzisha Idara hii itakayokuwa inasimamia mitandao yake yote ya kijamii.
6. Kuratibu na kusimamia shughuli zote za kijamii kama Mikutano, Makongamano,Semina, Warsha na mikusanyiko yote inayohusisha Viongozi wa Kanisa.
· Idara hii ina kazi ya kuhakikisha shughuli zote za kijamii zinazohusisha Viongozi wa Kanisa zinaandaliwa vizuri na kufanikiwa kama zilivyopangwa.
7. Kuwa Kiunganishi kati ya Kanisa na jamii
· Idara hii ina kazi kubwa ya kuunganisha jamii na Kanisa lao kupitia Viongozi wanaosimamia kanisa.
8. Kulisemea na kulijengea taswira nzuri Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini ndani ya jamii.
9. Kuratibu mikutano ya Waandishi wa habari na kushirikiana na vyombo vingine vya habari.
10. Kuinadi na kuitangaza miradi yote ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini.
11. Kushauri na kuzisaidia Idara zingine za kanisa katika maswala ya kiteknolojia na habari.
12.
Kuzisaidia shirika za Kanisa katika maswala
mbalimbali ya teknolojia na habari na kufikisha mbali Injili kupitia mahubiri,
uimbaji nk.
MALENGO YALIYOFANIKIWA MPAKA SASA.
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini kupitia Idara yake hii imefanikiwa katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo.
1. Kudhibiti uvujaji wa taarifa usiofuata taratibu za Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini.
2. Kuanzisha Mwamvuli wa kusimamia na kuendesha vyombo vyake vya habari unaoitwa Njiwa Media.
3. Kuanzisha na kuendesha vyombo vyake vya habari mtandaoni ambavyo ni
· Online Television {Njiwa Media}
· Online Radio {Njiwa Online Radio}
· Mitandao ya kijamii kama Facebook,Instagram,Whatsap na Thread {Njiwa Media}
4. Kuendesha Tovuti ya Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini {www.mctsp.org} pamoja na kusimamia uonekano wa Makumbusho yetu mtandaoni.
5. Kuunganisha jamii kubwa na Kanisa lao kupitia mitandao ya kijamii.
6. Kusimamia na kuratibu baadhi ya shughuli za Kikanisa kupitia baadhi ya Idara ikiwemo Idara ya Miradi na Ustawi wa Jamii.
7. Kujenga taswira nzuri ya Kanisa katika jamii
8. Kunadi na kutangaza miradi ya Kanisa vikiwemo vyuo vyetu, shule,Makumbusho na Butusyo Guest House.
9. Kushauri na kuzisaidia Idara zingine katika maswala mbalimbali yanayohusu teknolojia nk.
10. Kuzisaidia shirika zetu kupitia kwaya zao ili kuweza kufikisha injili mbali, ambapo mpaka sasa tayari kwaya kadhaa zipo mtandaoni na zingine zinaendelea kusaidiwa.
Gwamaka Jongo
S.L.P 32
Tukuyu
+255 761 325 346
jongogwamaka@gmail.com