Idara ya Vijana
Historia
Hapo mwanzo, idara hii iliitwa “Idara ya Vijana na shule ya Jumapili”. Shule ya Jumapili ilianzishwa na Robert Raikes kwa lengo la kufundisha watoto maskini kusoma, kuandika na kujifunza neno la Mungu.
Mwaka
1844, Bw. George William alikusanya vijana katika viwanda ili kuwafundisha neno
la Mungu. Baadaye alilipa jina shirika la vijana "Young Men Christian
Association” (YMCA). Mwaka 1861, Sr. Emma Kinnard alianzisha umoja wa wanawake
ulioitwa "Young Women Christian Association” (YWCA) kwa lengo la kuimba,
kupiga kinanda na kufanya kazi za nyumba. Mwaka 1875, hivi vyama viwili vilijiunga
na kuwa kundi moja. Mwaka 1959, chama hicho kiliingia Tanganyika na kiliitwa "Young
Christian Association” (YCA).
Kanisa la
Moravian liliikubali taasisi hii kama mwanachama wake mwaka 1958 katika Sinodi
ya Msangano Mbozi. Wakati huo, ofisi kuu ilikuwapo Rungwe na majimbo mawili
(Jimbo la Kusini na jimbo la Kusini-Magharibi) yalikuwa hayajagawanywa. Taasisi
ilikuwa kitengo cha "Vijana" chini ya Idara ya Elimu ya Kikristo
mwaka 1976 na kuzaliwa kwa Kanisa la Moravian nchini Tanzania jimbo la Kusini-Magharibi.
Malengo
Kitengo
cha Vijana kimegawanyika katika sehemu mbili. Kundi la kwanza linaitwa Vijana A
na lina vijana kati ya umri wa miaka 13 na 25. Kundi la pili linaitwa Vijana B
na lina watu wenye umri wa miaka 26 hadi 45 na watu wote walioolewa au kuoa
(bila kujali umri).
Lengo I: kuandaa vijana kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao na kueneza injili.
Lengo la II: kuendeleza mizizi ya maisha ya kiroho kwa vijana kwa njia ya ibada na masomo ya Biblia (binafsi na katika vikundi).
Lengo la III: kuendeleza umoja kati ya vijana katika Kanisa la Unitas Fratrum na kushirikiana na vijana wa makanisa mengine ndani na nje ya nchi.
Lengo la IV: kuhamasisha vijana kuwa waaminifu, kuwafundisha kuhusu uongozi wa Kikristo, na kukua na kuendeleza Ukristo maishani mwao.
Lengo V: kuwahimiza na kuwaruhusu vijana kufurahia muziki, michezo na maigizo.
Lengo la VI: kuwa na haki ya kuimba ibadani kama kundi kanisani.
Lengo la VII: kuwasaidia vijana wajitegemee kiuchumi.
Shughuli zetu
- Kufanya semina kwa vijana katika ngazi ya wilaya na jimbo
- Vikundi vya vijana katika ngazi ya usharika, wakati mwingine pamoja na kwaya
- Kambi ya vijana
- Kuwahimiza
vijana kuanzisha miradi inayozalisha mapato katika kilimo au usafirishaji na kuwafundisha
jinsi ya kuwaisimamia.
Matukio mbalimbali ya Idara ya Vijana.
Mapokezi ya wawakilishi wa vijana wa Kanisa la Moravian Dunia waliotembelea Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini na kupokelewa na Idara ya Vijana Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini mnamo tarehe 12/08/2022.
Mkuu wa Idara Mch. Dastan Mwasomola
Mawasiliano:
Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini
Idara ya Vijana
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania
Barua Pepe: dastanmwasomola@gmail.com
Simu: +255 765 902999