Idara ya Watoto yatima, Watoto Walio kwenye mazingira magumu na Wajane
Idara ya watoto yatima, watoto walio na mazingira magumu, wajane iliundwa rasmi mwaka 2007. Kabla ya hapo, kazi iliyofanyika ndani ya idara, ilikuwa chini ya idara ya wanawake na watoto.
Idara
imejikita zaidi kuunga mkono makundi yenye mazingira magumu katika jamii. Watoto yatima wanasaidiwa kwa
njia mbalimbali, kwa mfano kwa kuwalipia ada za shule na kuwapa vifaa vya
msingi vya shule kwa shule za sekondari, vituo vya mafunzo ya ufundi au vyuo
vikuu. Mara nyingi watoto huishi na ndugu zao ambao wanawasaidia. Kwa watoto yatima
wawili, huongezewa huduma za msingi, kama chakula, nguo na bidhaa za muhimu za
usafi. Ikiwa hakuna waangalizi, tunatoa malazi kwa yatima.
Kwa bahati mbaya,
bado kuna watoto wanaofanyiwa unyanyasaji nyumbani kwao, ndiyo maana tungali
tunawasiliana na wazee wa kijiji katika mkoa wetu. Mtoto anaponyanyaswa na
wazazi au waangalizi, tunajaribu kuingilia kati, kwa mfano kuwapeleka shule ya
bweni huko Lutengano.
Pia,
tunaandaa na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto walio na mazingira magumu
na yatima, kwa kuwaleta pamoja na wataalamu kutoka hospitalini au serikalini.
Idara inawasaidia watoto, wajane wa kike na wa kiume au waangalizi wakiwa na masuala ya kisheria.
Matukio hayo yanaripotiwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hutetea
haki za watu walio katika mazingira magumu mahakamani.
Kipengele
kingine muhimu katika kazi yetu ni kuwasaidia watunzaji kiuchumi. Tunaandaa
semina, ambapo tunawafundisha kuanzisha miradi inayozalisha kipato, kama kufuga
wanyama, kupanda miti ya parachichi au kufuga nyuki.
Pia
tunaendesha miradi yetu ya kuzalisha kipato, ambayo inatuwezesha kuwasaidia watoto
yatima na watoto walio na mazingira magumu na kazi yetu. Miongoni mwa mingine,
tuna mradi wa kuku, baadhi ya miti ya parachichi na msitu wa ekari mbili.
Inatia moyo
hasa tunapoona kwamba msaada wetu una matokeo chanja. Katika miaka iliyopita, tumeshuhudia
taarifa nyingi za mafanikio. Kwa mfano, watoto tuliowasaidia sasa wamemaliza
chuo kikuu na kupata kazi nzuri. wapo tayari kurudisha fadhira, kwa kuunga
mkono kazi ya kuwasaidia watu walio na maisha magumu kifedha.
Dhamira kuu
Kuwasaidia watoto yatima, watoto walio katika mazingira magumu na wajane wa kike na wa kiume katika kanisa la Moravian eneo la jimbo la Kusini, ili waweze kuishi maisha mazuri na ya kujitegemea.
Malengo
-
Kuwasaidia watoto yatima na watoto walio na shida kwa kuwapa elimu ya sekondari, mafunzo ya ufundi na Chuo Kikuu
Kuwawezesha watoto yatima na watoto walio na shida kwa kuwafundisha shughuli za kuzalisha kipato
Kutoa msaada wa kijamii kwa watoto yatima na watoto walio na maisha magumu (OVC) kwa kuwashauri
Kuwapunguzia kazi waangalizi / watunzaji.
Kutetea haki za OVC
- Kuongeza uelewa katika makanisa na jamii kuhusu mahitaji ya OVC
- Kuimarisha maendeleo ya kitaasisi na kibinadamu katika Idara ya OVC
HISTORIA YA MSICHANA ALIYELELEWA ,KUSOMESHWA NA IDARA YETU
Mkuu wa Idara: Mch. Nikwisa Mwakamele
Mawasiliano
Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini
Idara ya Watoto yatima, Watoto Walio na mazingira magumu na Wajane.
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania
Barua Pepe: nikukamele@yahoo.com
Simu: +255 753 700985