Idara ya Wanawake na Watoto
Idara ya
Wanawake na Watoto ilianzishwa mwaka 1952, na
kiongozi wa kwanza Annette Mbapa
Kabisa. Lengo kuu la idara lilikuwa kuimarisha mchango wa wanawake wanaoutoa
kanisani, kwa sababu idadi ya wanawake waliokuwa wakihudhuria kanisani ilikuwa
kubwa, lakini hawakuhusishwa kikamilifu kwenye nafasi za uongozi na kutoa
maamuzi. Jambo hilo limefanikiwa sana, Sasa, kuna wachungaji wa kike zaidi ya
53 na wainjilisti wawili wanaofanya kazi katika jimbo la Kusini , lakini bado
kunahitaji la idadi hiyo kuongezeka.
Zaidi ya hayo, idara ya wanawake pia inasaidia wanawake katika maisha yao ya kila siku. Tunafanya semina kuhusu mada mbalimbali, kama uwezo wa kimaendeleo, miradi ya kuzalisha kipato, ujasiriamali, uongozi, afya, kozi za Biblia na malezi ya watoto. Lengo ni kuwasaidia wanawake ili wawe huru zaidi. Idara pia inaendesha miradi yake ya kuzalisha mapato, kama upandaji wa misitu, kujenga maduka ya kufanyia biashara na mingine.
Pia tunaandaa
mikutano ya maombi mara kwa mara, ambapo wanawake huja na kuombea matatizo yao
ya kila siku na jamii nzima. Katika mikutano hii, tunakusanya pesa, ambazo
hutumiwa kulipa ada za shule kwa wasichana walio na shida na kuwapa vifaa vya
msingi vya shule. Pia tunatembelea mikutano mbalimbali kutoka mashirika
mengine, kama vile Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) au bodi ya kitaifa ya Kanisa
la Moravian nchini Tanzania (MCT).
Katika ngazi
ya usharika, idara ya wanawake na watoto inasaidia makundi ya walio na maisha magumu, kama wajane,
wagonjwa na wafungwa, kwa kuwapikia chakula na kuwapa msaada wa kiroho. Hii ni
njia ya kuonesha upendo na kuhubiri neno la Mungu kwa matendo.
Pamoja Tunaweza - "Together we can"
Pamoja Tunaweza ni moja ya miradi yenye mafanikio zaidi ya idara ya wanawake na watoto. Ni kundi la wanawake wapatao 10 ambao hutengeneza mikoba, mablanketi, mabegi, midoli na vitu vingine vingi. Vitu vinauzwa, kwa mfano katika Maua Café Mbeya, nyumba ya wageni ya Mbutusyo na katika ofisi ya idara ya wanawake.
Wanawake wote
wana mashine zao za kushonea, hivyo wanaweza kufanya kazi wakiwa nyumbani. Hiki
ni chanzo muhimu cha kupata kipato, kinachowasaidia kujitegemea na kuhudumia familia
zao.
Baadhi ya bidhaa zetu:
Uongozi
Mkuu wa Idara: Mch. Tupokigwe Mwamasangula
Msaidizi: Lucy Panja
Mawasiliano
Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini
Idara ya Wanawake na Watoto
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania
Simu: +255 763162120